Home KITAIFA ZIMAMOTO WATOA ELIMU KWA WALIMU NA WANAFUNZI KISARAWE

ZIMAMOTO WATOA ELIMU KWA WALIMU NA WANAFUNZI KISARAWE

Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Pwani limeendesha programu ya mafunzo ya kuzima moto na uokoaji kwa wanafunzi zaidi ya elf moja kutoka shule mbalimbali kata ya Kisarawe Pwani wakiwemo walimu pamoja na viongozi mbalimbali wamepatiwa mafunzo hayo yatakayosaidia kujiokoa pindi majanga yanapojitokeza iwe majumbani shuleni.

Akizungumza baada ya kuendesha zoezi la mafunzo ya kuzima moto na uokoaji yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Chanzige Kamanda wa jeshi la zima moto mkoa wa Pwani mrakibu mwandamizi wa jeshi la zimamoto JENIFA SHIRIMA amesema hivi sasa jeshi la zimamoto limeanzisha utaratibu wa kutembelea katika maeneo mbalimbali ili kutoa mafunzo ya namna ya kujikinga na majanga ya moto.

SHIRIMA mesema zoezi hilo si tu litwafikia wanafunzi tu bali litaendelea mpaka majumbani ili kuhakikisha elimu ya zima moto na uokoaji inamfikia kila mwananchi pamoja na taasisi mbalimbali za binafsi na serikali.

Ameongeza mesema jeshi la zima moto litaendelea na zoezi la kutoa elimu ya kujikinga na majanga ya moto kwa kutumia kifaa cha awali portable fire extinguisher na hiyo itakua ni muendelezo katika eneo mkoani Pwani ili kuwasaidia wananchi namna ya kujiokoa pindi majanga yanapoteka.

Mkuu huyo wa kikosi cha zima moto na uokoaji mkoa wa Pwani ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanatoa taarifa mapema pindi wanapokumbwa na majanga iwe ajali za barabarani na hata majanga ya moto ili kupata msaada wa haraka na wakitaalam.

Hata hivyo JENIFA SHIRIMA amemalizia kusema kuwa jeshi la zima moto siku zote lipo tayari kutoa msaada kwa wananchi pindi wanakumbwa na majanga na ndio maana wamekua wakitoa mawasiliano yao ili kudhibiti hatari zozte zinazoweza kujitokeza huku akitumia fursa hiyo kutaja nambari za simu ambazo ni 114 ambapo mwananchi atapiga na atapatiwa ushirikiano wa haraka.

Previous articleWAZIRI MKUU MAJALIWA AAGIZA KUZALISHA CHUMVI YENYE UBORA
Next articleTUME YA MADINI YATAKIWA KUWASAIDIA WAJASIRIAMALI KUPATA TEKNOLOJIA ZENYE GHARAMA NAFUU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here