Makamu wa Rais Dkt Isdor Mpango amelitaka jeshi la zimamoto a uokoaji nchini kufika kwenye matukio ya uokoaji kwa wakati ili kupunguza athari zinazotokana na majanga mbalimbali.
Dk Mpango ametoa agizo hilo wakati akifungua jengo la kituo kikuu cha Zimamoto Dar es Salam na kusisitiza kuwa jeshi hilo linadhamana kubwa ya usalama wa watu na mali zao na kupunguza athari zinazotokana majanga ya moto.
Ameaninisha malalamiko ya wateja kwa jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kuchelewa kufika katika matukio kwa wakati na magari yao kutokuwa na maji.
“Tunapoadhimisha miaka 59 ya Muungano hamna budi kujitafakari nilazima kuhakikisha mfumo wenu wa kiutendaji na haswa kutokana na ongezeko la watu na ukuaji wa miji ni lazima kuhakikisha jeshi letu linakuwa imara “
Dk Mpango amelitaka jeshi hilo kujiimarisha zaidi ili kuweza kukabiliana na majanga yakiwemo matetemeko ya ardhi,vimbunga na ajali za barabarani, angani na majini.
Naye Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunga amesema jengo la kituo kikuu cha Zimamoto na uokoaji Dar es Salaam lina thamani ya zaidi ya shilingi 4.9 bilioni.
Akiwa kwenye halfa hiyo ya ufunguzi wa jengo la kituo kikuu cha zimamoto na uokoaji Dar es Salaam ameeleza kuwa ujenzi huo ulianza mwaka 2010 na lilitarajiwa kuwa ofisi za makao makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kabla ya serikali kuhamia Dodoma.
“Jengo hilo lilipandishwa hadi kufikia ghorofa ya tatu na lilikuwa limegharimu shilingi 1.6 bilion ,June 2021 baada ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 2.3 kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa ghorofa tatu ili litumike kama kituo kikuu cha zimamoto Dar es Salaam” amesema
Hadi kukamilika kwa kituo hicho kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 4.9 na kinajumuisha majengo matatu yaani jengo la utawala, jengo la kuegesha magari na jengo la mazoezi ya askari lenye sakafu nne