Home KITAIFA ZAHANATI ZA KATA YA MKANGE HAZINA MANESI

ZAHANATI ZA KATA YA MKANGE HAZINA MANESI

Chama Cha Mapinduzi kata ya Mkange Bagamoyo mkoani Pwani kimeagiza kupelekwa haraka wahudumu wa afya wakike katika zahanati ya kijiji cha Gongo na zahanati ya kijiji cha Matipwili ambako wananchi wanapata shida kwa kukosa muhudumu wa afya kutoka kwa Wahudumu wa afya wa kike kijijini hapo.

Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Kata ya Mkange kuzungumza na Wananchi wa Kijiji cha Gongo Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mkange Abdallah Dimauya amesema katika vijiji vya Gongo na Matipwili hakuna kabisa Wahudumu wa afya mbali ya kukosekana kwa Wahudumu wa jinsia ya kike Kuna Madaktari tu.

“Hakuna Nesi kabisa hili jambo linatakiwa lifanyiwe kazi haraka kwani Kuna Madaktari wakiume wakiwa anamwa au wakisafiri huduma za afya hazipatikani na ukizingatia jinsia ya kike masuala ya uzazi hakuna anayeweza kuwahudumia kulingana na jinsia zao” alisema.

“Hiyo ni changamoto kubwa hasa kinamama wanakosa huduma, Kata ina Zahanati mbili za vijiji lakini vyote vina Madaktari wa kiume mmoja mmoja bila Wahudumu wa afya kabisa yaani Madaktari hao wakipata dharula yoyote tunakosa huduma”

“Wakienda kuchukua mishahara, wakiumwa au wakienda kwenye vikao vya kiutumishi Wananchi wa vijijini hivyo wanakosa huduma za afya hadi watakaporudi” amesema

Mwenyekiti huyo wa CCM Kata ya Mkange amemuagiza Diwani wa Kata hiyo Mohamed Gelegeza alishughulikie suala hilo haraka ili Wananchi wahudimiwe na vizuri haraka.

Akizungumzia idara ya elimu amesema kuna boma la Shule ya msingi lililojengwa tangu mwaka 2019 hadi Leo halijapata kuendelezwa mbali ya Wananchi kujitolea kwa asilimia kubwa kuanza kwa ujenzi wa Shule hiyo.

“Jamii imejitolea kwa kiasi fulani lakini kukosa kuendelezwa kwa boma la Shule Wananchi wanaona kama wametengwa jambo linawarudisha nyuma kujitolea kuchangia miradi ya maendeleo” amesema

Previous articleWAFANYABISHARA WAPIGWA MSASA JUU YA UTUNZAJI FEDHA
Next articleMABALOZI WA TANZANIA NJE YA NCHI KUIBEBA SEKTA YA MADINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here