Home KITAIFA WIZARA YA NISHATI YASIMAMISHA KAZI MAMENEJA WANNE WA TANOIL BAADA YA UKAGUZI...

WIZARA YA NISHATI YASIMAMISHA KAZI MAMENEJA WANNE WA TANOIL BAADA YA UKAGUZI WA NDANI

 

Wizara ya Nishati inaufahamisha umma kwamba, Serikali kupitia Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC imewasimamisha kazi Mameneja wa Kampuni ya TANOIL – Kampuni Tanzu ya TPDC, inayojihusisha na biashara ya mafuta. Kabla ya uamuzi huu, Serikali, kupitia Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, ilielekeza kufanyike ukaguzi mahsusi na wa kina wa uendeshaji wa kampuni ya TANOIL. Ukaguzi huo, uliofanywa na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, umeashiria ubadhirifu mkubwa katika uendeshaji wa Taasisi hiyo.

Waliosimamishwa ni Meneja Mkuu Mhandisi Kapuulya Musomba, Meneja wa Fedha na Utawala James Batamuzi, Meneja wa Hifadhi ya Mafuta Sudi Abdallah na Meneja wa Usambazaji na Uendeshaji Amour Marine.

Kutokana na hatua hiyo, Serikali, kupitia Bodi ya TPDC, imeweka uongozi wa muda wa kuendesha shughuli za Kampuni hiyo na kuiwasilisha ripoti ya ukaguzi kwa Taasisi Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa hatua stahiki. Pamoja na hatua hii, Bodi ya TPDC imeanza kutekeleza mapendekezo ya ripoti hiyo ya kuongeza udhibiti na kuandaa mkakati mpya wa kibiashara wa TANOIL. Itakumbukwa kwamba takriban mwezi uliopita, Serikali ilibadilisha menejimenti ya TPDC katika jitihada za kuimarisha uendeshaji wa Shirika ikiwemo usimamizi wa kampuni tanzu za Shirika.

 

Previous articleKIBAHA KUTOA ELIMU YA KIBOBEZI KWA WAJAWAZITO
Next articleBENKI YA DUNIA YAANZA ZIARA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA HEET

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here