Home KITAIFA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII YAFUNGUA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA

WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII YAFUNGUA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum imefungua kituo cha huduma za mawasiliano ya wizara na wateja(Jamii Call Center ) kitakachosaidia kupata taarifa, elimu, huduma na ufumbuzi dhidi ya changamoto mbalimbali ikiwemo ukatili kwa watoto mitandaoni.

Lengo la kituo hicho ni kuongeza wigo wa kuwahudumia watanzania kwa haraka,ufanisi,ufasaha na kumuondolea mteja adha ya kusafiri umbali mrefu na kutumia gharama zisizo za lazima kwenda kufuata huduma.

Akifungua kituo hicho leo Agosti 10 jijini Dodoma,Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dokta Dorothy Gwajima amesema moja ya changamoto kwenye utekelezaji wa wizara kuhusu huduma kwa jamii hasa iliyo mbali na wizara ni jinsi ya jamii kufikia taarifa na huduma za wizara kwa urahisi pale wanapohitaji,hivyo kituo hicho kitakuwa msaada mkubwa.

Amesema kuanzishwa kwa kituo hicho kutasaidia pia kutoa mwongozo na utaratibu dhidi ya manusura wa ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na watoto.

Dkt Gwajima ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa kisekta kutoa ushirikiano na kuunganisha nguvu za pamoja katika kutatua changamoto zitakazopokelewa na kutumia namba hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ya jamii yenye uhitaji mbalimbali kupatiwa huduma stahiki.

Previous articleRC MAKALLA ATAKA ELIMU ZAIDI ITOLEWE KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI
Next articleVIJANA 600 KUSHIRIKI KONGAMANO LA KITAIFA LA VIJANA KESHO DODOMA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here