Home KITAIFA WIZARA YA MADINI YADHAMIRIA KUONDOA CHANGAMOTO KWA WACHIMBAJI WA MADINI WAKUBWA NA...

WIZARA YA MADINI YADHAMIRIA KUONDOA CHANGAMOTO KWA WACHIMBAJI WA MADINI WAKUBWA NA WA KATI

Dkt. Biteko asikiliza mafanikio na kero za wachimbaji wa madini wakubwa na wa kati huu

Wizara ya Madini imedhamiria kuweka mipango thabiti kuhakikisha changamoto zilizopo kwenye Sekta ya Madini zinatatuliwa kwa lengo la kuongeza tija kwenye uzalishaji wa madini nchini.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko wakati akifungua kikao cha kujadili maendeleo, changamoto na kero zinazozikabili Kampuni kubwa na za kati zinazojishughulisha na uchimbaji wa madini nchini.

“Leo ni siku ya kuwasikiliza wachimbaji wakubwa wa madini na wa kati kama tunavyo wasikiza Wachimbaji Wadogo kama wanachangamoto gani ili tuweze kuzifanyia kazi lakini pia tunajiandaa na Mkutano wa Mkuu wa Kisekta wa Mwaka unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu,” amesema Dkt. Biteko.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Biteko amesema tayari serikali imerahisisha mazingira ya kikodi kwa wachimbaji wa madini ili kuondokana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokaza katika kutimiza wajibu yao.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Maji, Nishati na Madini kutoka Zanzibar Staibu Hassan ameipongeza Wizara ya Madini kwa hatua kubwa ambapo amesema wizara hiyo imekuwa mwalimu wa mataifa mengi kujifunza usimamizi bora wa shughuli za biashara na uchimbaji madini.

Naye, Mwenyekiti wa Chemba ya Migodi, Mhandisi Philibart Rweyemamu amesema Chama anachokiongoza kipo tayari kushirikiana na serikali ili kuondoa changamoto na kutoa suluhisho la kudumu katika sekta hiyo ili hatimaye kufikia lengo la kuchangia asilimia 10 kwenye Pato la Taifa ifikapo 2025.

“Kikao cha namna hii kitakuwa kinafanyika kila robo mwaka ili kutoa taarifa kwa serikali juu ya maendeleo ya shughuli zetu, kuueleza umma nini kinachofanyika pamoja na kuishauri serikali kitu gani tunafikiri kifanyike ili kurahisisha utendaji wa Sekta ya Madini,” amesema Mhandisi Rweyemamu.

Katika kikao hicho Kampuni tano za uchimbaji mkubwa wa madini zimetoa taarifa za utekelezaji wa miradi inayotekelezwa ikiwemo Kampuni ya Nyati Corporation, Sotta Mining, Tembo Nickel Corporation, Twiga Minerals na Faru Graphite Limited.

Previous articleWELEDI WATAKIWA WAKATI WA KUFANYA UTAFITI WA UKATILI DHIDI YA WATOTO.
Next articlePAROKO AUAWA KIKATILI KANISANI.. MUUAJI NAYE AUAWA NA WANANCHI _ MAGAZETINI LEO ALHAMISI JULAI 20/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here