Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Elimu Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Husna Sekiboko ameshiriki ufungaji wa wiki ya maadhimisho ya maonyesho ya Ubunifu wa Science na Technolojia yaliofanyika katika uwanja wa jamhuri jijini Dodoma.
Pamoja na shughuli zingine ameshiriki kutoa tuzo na zawadi kwa washindi walioshiriki mashindano hayo.
Wakati akihutubia kwa niaba ya kamati, ameomba maadhimisho hayo mwakani yafanyike katik mkoa wa Tanga na wizara imekubali ombi lake ambapo Waziri wa Elimu Prof Mkenda amewahakikishia washiriki kwamba mwakani watahamia Mkoa wa Tanga kuitikia wito wa Mhe Sekiboko.
Sekiboko alisisitiza kuwa kufanyika kwa maadhimisho hayo katika mkoa wa Tanga kutasaidia kuwapa fursa wananchi kushiriki kwa wingi ili kujifunza, kufanya biashara na kujiongezea kipato pamoja na kupata fursa ya kuibua vipaji, ubunifu na ugunduzi mbalimbali.
“Zipo bunifu mbalimbali ambazo mpaka sasa zimewalipa watu mbalimbali mpaka wamefungua makampuni makubwa ya biashara kupitia MAKISATU” Alieleza Makamu Mwenyekiti huyo.
Maadhimisho hayo yamewashirikisha wananchi kutoka mikoa yote ya Tanzania, Vyuo vikuu, vyuo vya ufundi, shule mbalimbali na wagunduzi binafsi.