Home KITAIFA WIKI YA MADINI KITAIFA KUFANYIKA MWANZA MEI 3-10

WIKI YA MADINI KITAIFA KUFANYIKA MWANZA MEI 3-10

 

 

Wachimbaji wadogo wa madini zaidi ya 2,000 kutoka mikoa mbalimbali nchini wanatarajia kukutana Mei 3 hadi 10, mwaka huu 2023 jijini Mwanza kuadhimisha wiki ya madini kitaifa na kongamano la wachimbaji wa madini Tanzania ambao watazungumzia masuala ya uchimbaji.

 

Pia wachimbaji hao watahudhuria mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania(FEMATA) utakaofanyika Mei 10 katika ukumbi wa Rock City Mall jijini hapa.

 

Hayo yameelezwa na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) John Bina, kuhusu maandalizi ya wiki ya madini na kongamano hilo ambalo kitaifa litafanyika jijini Mwanza kwenye viwanja vya Rock City Mall.

 

“Maandalizi yanakwenda vizuri kabisa, kongamano hilo litawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya madini kutoka ndani na nje ya nchi litaambatana na mambo tofautitofauti ikiwemo maonesho ya teknolojia za kisasa za uchimbaji madini, elimu ya mikopo ya uchimbaji kutoka taasisi za fedha na elimu ya afya kwa ajili ya kutunza afya na mazingira kwenye nchi yetu, John Bina Rais Femata.

 

“Kongamano la wachimbaji litafanyika Mei 9, 2023 ambapo tunatarajia kupata mgeni rasmi kiongozi wa kitaifa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania Mheshimiwa Majaliwa Kasim Majaliwa, na litafuatiwa na usiku wa madini pale viwanja vya Hotel ya Malaika ambao utaambatana na kutoa tuzo za aina mbalimbali kwa watu walioshirikiana vyema na FEMATA katika kufanikisha shughuli za uchimbaji na waliolipa tozo na kodi zao vizuri,”alisema Bina na kuongeza.

 

Aidha Rais Bina amesema, leo Mei 4 mwaka huu siku ya Ahamis Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo ambapo atafungua maonyesho hayo ambayo yatafanyika kwenye viwanja vya Rock City Mall.

Maadhimisho hayo ya mwaka huu yana kauli mbiu isemayo, amani iliyopo Tanzania itumike kuwa fursa ya kiuchumi na Tanzania kuwa kitovu cha biashara ya madini Africa.

Previous articleSIGARA ZENYE BANGI ZAKAMATWA ZIKIINGIZWA NCHINI_ MAGAZETINI LEO ALHAMISI MEI 04/2023
Next articleTUONGEZE JITIHADA ZA KUFANYA UTAFITI WA KUTOKOMEZA MIMEA VAMIZI- JENARELI VENANCE MABEYO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here