Home KITAIFA WENYE UHITAJI WAPEWA MSAADA KUFURAHIA KRISMASI KATA YA LUBONDE

WENYE UHITAJI WAPEWA MSAADA KUFURAHIA KRISMASI KATA YA LUBONDE

News

Njombe

Diwani wa kata ya Lubonde iliyopo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Edger Mtitu ametoa misaada ya Kibinadamu vikiwemo vyakula kwa watu wenye mahitaji maalumu katika kata hiyo ili waweze kufurahia kwa pamoja sikukuu ya Krismasi

Akizungumza mara baada ya kuwatembelea majumbani kwao na kisha kukabidhi msaada wa vyakula ukiwemo mchele,Mafuta na fedha Mtitu amesema ni kutokana na kundi hilo kusahaulika kwa kiasi kikubwa na kudai kwamba kupitia kidogo hicho watakwenda kusherekea kwa furaha na amani sikukuu.

“Kwa bahati mbaya sana kundi la watu wenye mahitaji maalumu linasahaulika kwasababu halina utamaduni wa kutembea na kuchangamana na makundi mengine hivyo mahitaji hayo yatarejesha furaha kwao na kuwataka wadau wengine kulikumbuka kundi hilo”amesema Edger Mtitu Diwani wa Luponde

Kuhusu watu aliowalenga katika misaada hiyo iliyosambazwa kwenye vijiji vinavyounda kata ya Lubonde diwani huyo amesema ni Yatima,Wazee ,walemavu na watu waishio katika mazingira magumu akiwa na lengo la kutoa sadaka kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kwa ushirikiano Mkubwa anaoupata kwa wananchi katika shughuli za maendeleo.

Katika hatua nyingine Mtitu ametoa onyo kwa watu wanaowatenga watu wenye mahitaji maalumu na wanaoishi katika mazingira magumu na kuwataka watu wenye kipato na wenye mapenzi mema kuendelea kuyakumbuka makundi hayo yanatotengwa mtaani.

Kwa upande wake mtendajiwa kata ya Lubonde Anna Mwalongo amemshukuru diwani huyo kwa kuwashika mkono katika kipindi hiki cha sikuu watu wenye mahitaji maalumu na waishio katika mazingira magumu na kisha kuwaomba wadau wengine kuja kusaidia wengine kwasababu watu hao wapo wengi kwenye kata hiyo.

“Katika kata yangu kuna watu wengi wenye mahitaji maalumu hivyo tunaomba kama kuna wadau wengine wanaoweza kuja kuwasaidia”amesema Anna Mwalongo Mtendaji Lubonde

Nao baadhi ya wanufaika akiwemo Edner Mgaya na Nathan Mnyambwa wameshindwa kuzuia hisia zao kwa msaada huo wa chakula na fedha kwa ajili ya sikukuu na kisha kuomba wadau wengine kuwasaidia mahitaji mengine

Previous articleASKOFU KASSALA: NI BORA NIBARIKI JIWE LAKINI SIO MASHOGA/WASAGAJI
Next articleUTEKELEZAJI MRADI WA UMEME WA JULIUS NYERERE (JNHPP) WAFIKIA ASILIMIA 94.78

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here