Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu
amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika upatikanaji wa umeme wa uhakika katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.
Waziri Ummy amesema hayo mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kwenye maonyesho ya Wiki ya Nishati inayoendelea kufanyika JIjini Dodoma katika viwanja vya Bunge.
Amempongeza pia Waziri wa Nishati Mhe. Januari Makamba na watendaji wote katika Sekta ya Nishati kwa kuendelea kuhakikisha watanzania wanapata nishati ya umeme ambayo pia inasaidia katika uboreshaji wa huduma za afya
“Upatikanaji wa umeme wa uhakika unasaidia pia katika kuboresha huduma za matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa uharaka zaidi kwa kutumia vifaatiba.” amesema Waziri Ummy.