Home KITAIFA WAZIRI ULEGA: WAFUGAJI WANAOINGIZA MIFUGO MASHAMBANI KWA MAKUSUDI NI WAHALIFU

WAZIRI ULEGA: WAFUGAJI WANAOINGIZA MIFUGO MASHAMBANI KWA MAKUSUDI NI WAHALIFU

Mkuranga.

Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema wafugaji wanaoingiza Mifugo mashambani makusudi ni wahalifu wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Amesema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Nyandutulu Kata ya Nyamato wilayani Mkuranga mkoani Pwani akionyeshwa na uongozi wa Kata wakiwa na Wananchi eneo la kujenga shule ya Sekondari ya Kata ya Nyamato huko Nyandutulu.

Amesema hayo baada ya Mwenyekiti wa kitongoji cha Kazolo Ashura Mkele kulalamikia Mifugo kuingizwa mashambani makusudi katika mashamba ya wakulima katika kitongoji ambacho hakijapangiwa kupokea Mifugo.

Ashura amesema Wafugaji wamekuwa wakiwakatisha tamaa wakulima kwa kuwa kero kwa wakulima katika kitongoji hicho kwa kuingiza Mifugo mashambani makusudi jambo ambalo husababisha kukosa uhakika wa chakula katika mwaka.

Akijibu malalamiko hayo Ulega aliwaagiza Watendaji wa vijiji na vitongoji wahakikishe Wafugaji wanaoingiza Mifugo mashambani makusudi wawasimamie ili kuwadhibiti sambamba na kuhakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi yao.

Ulega amesema kitendo wanachofanya cha kuingiza Mifugo mashambani ni uvunjaji wa sheria za Nchi hivyo lazima wadhibitiwe kwa hatua kali za kisheria.

“Eneo ambalo halikutengwa kwaajili ya ufugaji lazima lidhibitiwe iwe lazima Mifugo kutoingia kwenye eneo hilo na kama eneo hili halikupangwa kupokea Mifugo hakikisheni iwe ni marufuku Mifugo kuingia katika eneo hili” amesema Ulega.

Amesema “Hakuna kuoneana aibu Wafugaji wenye tabia kama hizo wachukuliwe hatua za kisheria kwani tabia kama hizo ni kutiana njaa na umasikini haiwezekani mtu achukue ng’ombe wake makusudi na kuwaingiza kwenye shamba la mtu mwingine huo ni ualifu simamieni haki itendeke”

Aidha alimtaka Diwani wa Kata ya Nyamato Faraji Kisebengo kumpa Waziri huyo taarifa iwapo atabaini Kuna mianya ya utoaji na upokeaji wa rushwa wampe taarifa aongeze nguvu za ushughulikiaji.

“Ikiwa mtaona Kuna mianya ya rushwa nijulisheni haraka yaani mnijulishe tu kwamba tobo lipo pale ndio panapovuja kukwamisha agizo lako hata tukifanya usimamizi mzuri wa namna gani jambo halitekelezwi kwasababu ya tobo Hilo nielezeni tushughulikie hilo tobo” amesema.

Naye Mtendaji Kata ya Nyamato Ally Akida amesema tayari wameanza kushughulikia kero hiyo ingawa changamoto wanayokutana nayo ni kwamba Wafugaji wengi wanaofanya makosa hayo hawakai katika Kata ya Nyamato wao hutokea katika Kata jirani ya Lukanga.

Previous articleNIMEPATA MKE TAJIRI BAADA YA KUTUMIA DAWA YA MVUTO WA KIMAPENZI
Next articleBAWACHA KAGERA WAJIBU KAULI ZA M/KITI WA UWT TAIFA DHIDI YA MBOWE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here