Home KITAIFA WAZIRI ULEGA AAHIDI SERIKALI KUBORESHA MACHINJIO YA MBALIZI

WAZIRI ULEGA AAHIDI SERIKALI KUBORESHA MACHINJIO YA MBALIZI

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ametembelea na kukagua Machinjio ya Ng’ombe katika eneo la Utengule Kata ya Utengule Usongwe Mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi Wilayani Mbeya na kuahidi Wizara kushirikiana na Halmashauri ya Mbeya kuhakikisha machinjio hiyo inakuwa ya kisasa zaidi.

Pamoja na ukaguzi huo pia Waziri huyo amekagua eneo la Tanganyika Packers katika eneo la Mbalizi II.

Katika ziara hiyo Waziri wa mifugo ameitaka Halmashauri ya Mbeya na wananchi kushirikiana kulinda eneo la machinjio ili isiingiliwe na watu kwa maslahi binafsi.

Akizungumza mbele ya Waziri wa Mifugo, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya Stephen Katemba, amesema pamoja na njia nyingine, Machinjio ya Utengule Mji mdogo wa Mbalizi inahitaji fedha zaidi ya shilingi Billion moja ili kuboreshwa zaidi kufikia hadhi ya kuchinja na kusindika nyama kwa ajili ya mji mdogo wa Mbalizi na Mbeya mjini.

Kuhusu hilo, Waziri wa Mifugo na uvuvi Abdalah Ulega amechukua maombi hayo ya Halmashauri ya Mbeya na kuahidi kwenda kuangalia njia bora ya kufanya ili kuboresha machinjio hayo katika kukuza uchumi wa wananchi na Serikali na kuitaka Serikali ya Wilaya na wananchi kuwa walinzi wa eneo la Machinjio hiyo (Utengule).

Machinjio ya Utengule ndio tegemeo kwa wananchi ndani na nje ya Mji wa Mbalizi na pia inaiingizia Serikali mapato kupitia shughuli za machinjioni hapo ambapo wizara imeahidi kufanyia kazi ushauri uliotolewa katika kuboresha machinjio hayo kuwa ya kisasa zaidi hata kuchinja na kusindika nyama.

Previous articleMOROGORO KUJA NA MKAKATI WA KUKUZA PAMBA NA KOROSHO
Next articleMHE BITEKO AMPA HEKO RAIS SAMIA UJENZI WA ICU WILAYA YA BUKOMBE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here