Home KITAIFA WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI

WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI

Waziri Mkuu mstaafu awamu ya nne Mizengo Kayanza Peter Pinda amefungua maonesho ya wakulima,wafugaji na wavuvi kanda ya Mashariki yanayofanyika katika viwanja vya Nanenane mkoani Morogoro.

Akizungumza na wananchi katika eneo yanapofanyika maonesho hayo Mstaafu Pinda amesema, kuwa licha ya Morogoro kuzalisha vyakula vingi lakini ni miongoni wa Mikoa yenye tatizo la udumavu ambapo Mkoa huo una asilimia 30 huku Mkoa kinara kwa udumavu ukiwa iringa kwa asilimia 56.9%

Pinda amesema kuwa tatizo la udumavu huo hasa Kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano linasababishwa na wazazi kuuza mazao yote badala ya kuyatumia kwa chakula.

Aidha kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Malima amesema, malengo ya Mkoa wa Morogoro nikuwa Mkoa wa kimkakati katika kilimo nchini.

Malima ameongeza kuwa takwimu za mwaka jana katika uzalishaji wa mpunga Mkoa wa Morogoro ulizalisha mpunga tani laki tisa ambapo matarajio ya msimu ujao ni kuzalisha tani zaidi.

Nae Abubakari Kunenge mkuu Mkoa wa Pwani ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Nanenane kanda ya Mashariki amesema mwaka huu wanategemea washiriki wa maonesho hayo kufikia 75 elfu ikilinganishwa na mwaka jana ambapo washiriki walikuwa elfu hamsini.

Maonesho ya Nanenane kanda ya Mashariki yanayofanyika Mkoani Morogoro yanajumuisha Mikoa minne ambayo ni Pwani,Tanga, Dar es salaam pamoja na mkoa wa Morogoro.

Previous articleALIYETUKANA VIONGOZI TIKTOK AKAMATWA, POLISI WATOA ONYO KALI
Next articleMBUNGE SEKIBOKO ATAKA WATOTO WALINDWE DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here