Home KITAIFA WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AZINDUA BARAZA LA KUTOKOMEZA MALARIA NCHINI

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AZINDUA BARAZA LA KUTOKOMEZA MALARIA NCHINI

 

Na WAF – Dsm

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezindua rasmi Barala la Taifa la Kutokomeza Malaria nchini ambalo litasaidia kuhamasisha upatikanaji wa rasilimali kutoka katika vyanzo vya ndani ambavyo vitawezesha kupunguza pengo la uhitaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza afua za udhibiti wa Malaria.

 

Halfa ya uzinduzi wa Baraza hilo imefanyika leo kwenye maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani ambayo Kitaifa yameadhimishwa Jijini Dar Es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

 

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Samia Suluhu Hassan ameunda Baraza hili lenye wajumbe 19 ili kuongeza hamasa zaidi za mapambano dhidi ya malaria na kusaidia kwenye ukusanyaji wa rasimali mbalimbali kwa ajili ya mapambano hayo na kufanikiwa kuutokomeza ifikapo mwaka 2030” amesema Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

 

Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Leodigar Tenga kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo ambalo limesheheni watu mashuruhi wenye ushawishi ndani ya jamii wakiwemo, Mfanyabiasha maarufu Said Salim Bakhresa, Wasanii Naseeb Abdoul (Diamond Platmunz), Zena Mohammed (Shilole) Viongozi wa Dini wakiwemo Askofu Fredrick Shoo na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abooubakar Zuberi pamoja na wajumbe wengine kutoka taasisi za fedha na asasi za kijamii.

 

“Baraza hili litachangia sana katika kupunguza pengo la upatikanaji wa rasilimali na kuleta tija katika mapambano dhidi ya malaria na tunaamiji kwa mchanganyiko wa wajumbe waliopo tutapata mafanikio makubwa sana” amesema Waziri Mkuu

 

Awali akizungumza, Waziri wa Afya Mhe. Ummy amesema uanzishwaji wa baraza hilo ni sehemu ya kutatua changamoto ya upatikanaji wa rasilimali za kutekeleza baadhi ya afua za Malaria.

 

“Uundwaji wa Baraza hili unatokana na maazimio ya Viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kwenye mikutano yao ya mwaka 2016 na 2017, ambapo kwa pamoja waliazimia kuimarisha mikakati ya kudhibiti Malaria ili kufikia lengo la kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030” Amesema Waziri Ummy

Previous articleMAAMBUKIZI YA MALARIA YAMEPUNGUA ASILIMIA 14 KATAVI
Next article‘MAJI BWAWA LA NYERERE YAFIKIA MITA ZA UJAZO BILIONI 6’ – WAZIRI MAKAMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here