Home KITAIFA WAZIRI MKUU MAJALIWA AOMBA KUSITISHWA MGOMO KARIAKOO

WAZIRI MKUU MAJALIWA AOMBA KUSITISHWA MGOMO KARIAKOO

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasihi wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo kufungua maduka ili kuendelea na biashara wakati Serikali ikishughulikia changamoto za wafanyabiashara zao.

 

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa wito huo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa soko hilo ambao wamekuwa katika mgomo kwa zaidi ya saa tisa “ hata kama kuna matatizo bora shughuli zikawa zinaendelea ili tusiendelee kuwapoteza wateja wetu kutoka nje na ile hadhi ya kimataifa iweze kuendelea.”

 

Hata hivyo amesitisha utaratibu wa Kamata kamata huku akieleza inachangia kuua biashara na maduka mengi yatafungwa.

“Leo TRA Rais amesema kodi za miaka mitano huko nyuma mziache, nyie mnadai barua kwa watu wa Kariakoo, hivi mtu wa Kariakoo ataipata wapi barua ya Rais? halafu unamuambia mfanyabiashara kwamba hilo ni agizo tu la kisiasa lilitamkwa na Rais wako; hiyo ni dharau na ningetamani nimjue ni nani huyo, tushughulike naye mara moja”-Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

 

“Mfanyabiashara anadaiwa kodi, mpelekee notisi, na kama kweli ameridhia kufanya biashara na anajua ukifanya biashara ni lazima ulipe kodi, atalipa kodi ili afanye biashara.” amesema

Previous articleKATIBU MKUU WA CCM AFUNGUA UKUMBI WA MIKUTANO WA CCM JIMBO LA BUKOMBE
Next articleWATUHUMIWA MAUWAJI YA DK ISACK, MILEMBE WAKAMATWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here