Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa jamii kuwa walinzi wa watoto na kujijengea utamaduni wa kutoa taarifa vinapotokea vitendo vya ukiukwaji wa maadili.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya mtoko na mama ambapo amesisitiza maadili ndio utambulisho wa kila mmoja katika jamii.
“Watanzania wote tushirikiane kukemea vikali vitendo vyote vya mmomonyoko wa maadili kwa kisingizio chochote,Mkataa kwao ni Mtumwa, sisi ni watu huru” amesema Waziri Mkuu Majaliwa
Aidha amewasihi Viongozi wa madhehebu ya dini kuendelea kuwalea watoto kiroho na kuwahimiza kuacha vitendo visivyofaa kwa kuwa havimpendezi Mwenyezi Mungu.