Home KITAIFA WAZIRI MCHENGERWA AHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA KUGAWA MITUNGI...

WAZIRI MCHENGERWA AHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA KUGAWA MITUNGI YA GESI 900 KWA MAMA LISHE WA RUFIJI

Na Mwandishi Wetu,

BAADA ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuzindua Mpango wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Wanawake wa Bara la Afrika, Mbunge wa jimbo la Rufiji mkoani Pwani ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEM) Mohamed Mchengerwa kwa kushrikiana na Oryx Gas ameamua kuunga mkono hatua hiyo kwa kugawa bure mitungi ya gesi ya Oryx 900 na majiko yake kwa mama lishe wote wa wilaya ya Rufiji.

Kwa mujibu wa Waziri Mchengerwa amesema matumizi ya kuni na mkaa yamekuwa yakichangia uharibifu wa mazingira na kusababisha kero mbalimbali nchni, hivyo kutumia nishati safi ya kupikia kutapunguza uharibu wa maazingira lakini pia kulinda afya za wanawake na watoto ambao ndio waathirika wakubwa wa moshi wa kuni wakati wa kupika.

Waziri Mchengerwa amegawa mitungi hiyo wilayani Rufiji katika sherehe za kukumbuka mchango wa mwanamama shupavu Bibi titi Mohamedi ambaye katika enzi za uhai wake alijitoa kwa hali na mali kupigania uhuru na ukombozi wa Taifa ambapo pia viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo Mwenyekti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) Mary Chatanda, viongozi Mkoa wa Pwani pamoja na maofisa wa Oryx wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wao Benoit Araman wamehudhuria.

Amesema uamuzi wa kugawa mitungi kwa mama lishe wote wa wilaya ya Rufiji unalenga kutambua mchango mkubwa wa wanawake wa jimbo hilo katika kujiletea maendeleo na kutunza mazingira kwa kutumia nishati safi ya kupikia na kuachana na kutumia kuni.

“Tunatambua mchango mkubwa wa kundi hili la mama zetua na dada zetu ambao wanajihusisha na shughuli za nama lishe, hivyo kwa kushirkiana na viongozi wenzangu wakiwemo madiwani tulikubabaliana tutafute mitungi ya gesi ya orxy na kisha kuwapatia mama lishe wote wa wilaya ya Rufiji wako 1300. Hivyo leo kwa kushirikiana na Kampuni ya Oryx tunagawa bure mitungi 900 yakiwa na majiko yake bure na mitungi iliyobakia tutagwa hivi karibuni.

“Tunataka kuona mama lishe wa wilaya ya Rufiji wanakuwa sehemu ya kutunza mazingira kwa kupikia nishati safi lakini wakati huo huo kuwalinda dhidi ya athari zinazotokana na kuvuta moshi wa kuni wakiwa katika shughuli zao za kila siku,” amesema Mchengerwa huku akisisitiza kuwa umefika wakati wa wananchi kuungana na serikali inayoongozwa na Rais Samia katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuendelea kulinda mazingira yetu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Araman amesema wamefurahi kupeleka nishati safi ya kupikia kwa wananchi wa wilaya ya Rufiji na kugusa kundi hilo muhimu katika jamii ambalo shughuli zao za kila siku zinahitahi kupata nishati ya kupikia.

“Kupika katika gesi ya Oryx ni kulinda mazingira kwa kuacha kukata miti na zaidi ya yote ni kulinda afya ya wanawake na watoto ambao wamekuwa wakiathirika kwa kuvuta moshi mbaya unaotokana na kuni. Rais wetu Mama Samia amejipanga kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata nishati safi ya kupikia ifkapo 2032.

“Katika mkutano wa Dubai ,Rais Samia amezindua Mpango wa Nishati safi ya kupikia kwa wanawake wa Afrika.Oryx Gas tutaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhamasisha matumizi ya nishati safi ua kupikia kwa kugawa bure mitungi ya gesi na majiko yake.

“Hadi leo hii Oryx tunajivunia kwa kutoa mitungi zaidi ya 15000 yenye thamani ya zaidi ya Sh.bilioni moja katika kipindi cha kuanzia mwaka 2022 mpaka sasa kupitia mpango wetu wa kuhamasisha nishati safi ya kupikia ikiwa ni sehemu ya kuungana na Rais Samia katika kuhamaisha wananchi kutumia nishati hiyo. Ahadi yetu kwa serikali tutaendelea kuhamasisha kwa kugawa bure mitungi na majiko kwa makundi mbalinbali ya wananchi

Akieleza zaidi amesema kutumia nishati safi ya kupikia Kuna faida kubwa za kiafya na kimazingira lakini wakati huo huo inatoa nafasi kubwa ya watoto kupata nafasi ya kwenda shule kupata elimu badala ya kutumia muda mwingi kwenda kukusanya kuni. ”Nakushukuru Waziri Mchengerwa kwa kufanikisha mpango huu wa nishati safi ya kupikia kwa wnanchi wa Rufiji kwa kuwapatia mitungi ya gesi 900″

Wakati huo huo kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Pwani, Jenipher Shirima, ametumia nafasi hiyo kuelezea kwa kina kuhusu namna nzuri ya kutumia nishati ya gesi katika kupikia ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea iwapo itatumika vibaya.

“Ni muhimu kwa wanawake na wananchi wote kuzingatia matumizi bora ya majiko ya gesi na kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya moto na pale yanapotokea kutoa taarifa mapema kwa jeshi hilo hatua zichukuliwe haraka.”

Previous articleGGML YATOA MILIONI 17 KUNG’ARISHA ATF MARATHON
Next articleKAMPUNI YA ORYX TANZANIA YAGAWA BURE MITUNGI 15,000 PAMOJA NA MAJIKO YAKE YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1 NDANI YA MIEZI 12

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here