Home KITAIFA WAZIRI MBARAWA AELEZA SABABU YA BANDARI ZA ZANZIBAR KUTOKUWEPO KATIKA MKATABA WA...

WAZIRI MBARAWA AELEZA SABABU YA BANDARI ZA ZANZIBAR KUTOKUWEPO KATIKA MKATABA WA UENDELEZAJI WA BANDARI

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema Zanzibar haipo katika makubaliano yaliyoingiwa na serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji kwenye bandari kwa sababu sheria iliyoanzisha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), inaipa jukumu kusimamia na kuendesha bandari zote za Tanzania Bara pekee.

Alisema jijini Mwanza alipokutana na kuzungumza na viongozi mbalimbali wa bandari na kutoa ufafanuzi juu ya makubaliano hayo ya ushirikiano katika bandari. Profesa Mbarawa alisema kusainiwa kumezusha maswali kwa wananchi wakihoji sababu za Zanzibar kuhusika kwenye mkataba huo.

“Zanzibar haipo kwa sababu Sheria namba 17 ya mwaka 2004 ya kuundwa TPA, inaipa jukumu la kusimamia na kuendesha bandari za Tanzania Bara, na si Zanzibar, “alisema Mbarawa.

Previous articleWANANCHI WATAKIWA KUZINGATIA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA
Next articleCCM MBEYA VIJIJINI YACHARUKIA UZEMBE FEDHA ZA RAIS SAMIA MIRADI YA MAJI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here