Home KITAIFA WAZIRI BASHE AWEKA WAZI MPANGO WA WIZARA YA KILIMO KUIFANYA WILAYA YA...

WAZIRI BASHE AWEKA WAZI MPANGO WA WIZARA YA KILIMO KUIFANYA WILAYA YA MAKETE KUWA YA MFANO KWENYE KILIMO CHA NGANO

Njombe

Serikali kupitia Wizara ya kilimo inatarajia kuifunga wilaya ya Makete iliyopo mkoani Njombe kwenye uzalishaji wa mazao mengine na kubakia na kilimo cha zao la Ngano pekee mara baada ya kukamilika kwa zoezi la upimaji wa ardhi ili kuwezesha eneo la wilaya hiyo kuwa ya mfano kwenye kilimo cha ngano nchini.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameeleza hayo wakati akiongea kwa njia ya simu na wananchi wa wilaya ya Makete kwenye kikao cha maandalizi ya msimu wa kilimo cha ngano 2023 – 2024 kilichoitishwa na mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka wilayani humo.

“Tutaifunga wilaya ya Makete baada ya zoezi letu la upimaji ardhi kukamilika kuwa ni production area ya Ngano peke yake,mtauliza Mahindi tutakula wapi,tutakapoifunga tutatafuta solution ya Mahindi kwasababu mtakuwa mnahela mtanunua Mahindi kwa hiyo tutalifanyia eneo lenu kama eneo la majaribio”amesema Waziri Bashe

Aidha Waziri bashe amemuagiza mkurugenzi mkuu wa bodi ya mazao ya nafaka na mazao mchanganyiko (CPB) John Maige kuhakikisha bodi inanunua Ngano kwa ghalama ya shilingi 1000 kwa kila kilo moja ya Ngano.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amesema tayari serikali kupitia wakala wa mbegu (ASA) imeridhia kutoa tani 1000 ya mbegu za ngano ambapo mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Makete Willium Makufwe akibainisha kuwa tayari halmashauri hiyo ipo kwenye hatua kubwa za upimaji wa ardhi pamoja kuanza kilimo hicho ambapo pia wakitarajia kufikia makusanyo ya bilioni 6,900,000,000.00 kwenye zao la ngano peke yake itakapofika mwaka 2025 – 2026

Previous articleJAMII IENDELEE KUJIANDAA KUJIKINGA NA MAAFA- DKT YONAZI
Next articleWIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, FEDHA KUSHIRIKIANA KUELIMISHA JAMII

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here