Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema takwimu zinaonesha kuwa mahitaji ya maji nchini kwa sekta mbalimbali mwaka 2022 yalikuwa ni wastani wa mita za ujazo bilioni 62 na yanatarajiwa kuongezeka na kufikia mita za ujazo bilioni 80.2 mwaka 2035.
Aweso ameyasema hayo bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya maji ambapo amesisitiza mahitaji hayo yataendelea kuongezeka kutokana na ongezeko la watu, ukuaji wa shughuli za uzalishaji mali katika sekta mbalimbali hususan kilimo cha umwagiliaji, uzalishaji wa umeme, uzalishaji viwandani, utalii, uchimbaji madini, ufugaji, uvuvi na wanyama pori.
Kwa upande mwingine, amebainisha uharibifu wa mazingira hususani kwenye vyanzo vya maji, uhaba wa mvua unaotokana na mabadiliko ya tabianchi na matumizi mabaya ya maji husababisha kupungua au kukauka kwa maji katika vyanzo.
18.
Mwaka wa fedha 2022/2023, Wizara ya Maji iliidhinishiwa 709,361,607,000 na kati ya fedha hizo Shilingi 51,462,269,000 zilikuwa ni fedha za matumizi ya kawaida na Shilingi 657,899,338,000 zilikuwa ni fedha za maendeleo.