Home KITAIFA WAZIRI AWESO AOMBA BIL.756.2 WIZARA YA MAJI 2023/24

WAZIRI AWESO AOMBA BIL.756.2 WIZARA YA MAJI 2023/24

Waziri wa Maji Juma Aweso ameliomba bunge kuidhinisha jumla ya Shilingi 756,205,106,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2023/24.

Akiwasilisha mapendekezo hayo bungeni Aweso amesema Kati ya fedha hizo, matumizi ya Kawaida ni Shilingi 60,375,474,000 ambapo Shilingi 18,035,561,000 sawa na asilimia 29.87 ni kwa ajili ya kugharamia Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi 42,339,913,000 sawa na asilimia 70.13 ni kwa ajili ya kulipa Mishahara (PE) ya watumishi wa Wizara, RUWASA na Chuo cha Maji.

Amesema jumla ya bajeti ya maendeleo ni Shilingi 695,829,632,000 ambapo kati ya fedha hizo, Shilingi 407,064,860,000 sawa na asilimia 58.50 ni fedha za ndani na Shilingi 288,764,772,000 sawa na asilimia 41.50 ni fedha za nje.

Previous articleDKT. YONAZI AONGOZA KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU CHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA
Next articleWAZIRI AWESO: UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA KUONGEZEKA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here