Home KITAIFA WAWILI AKIWEMO MCHUNGAJI WASHIKILIWA NA POLISI KWA KULAGHAI MCHAWI KADONDOKA NA UNGO...

WAWILI AKIWEMO MCHUNGAJI WASHIKILIWA NA POLISI KWA KULAGHAI MCHAWI KADONDOKA NA UNGO KANISANI KWENYE MKESHA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashilika watu wawili akiwemo Emanuel Paul Karata (35) mchungaji wa kanisa la

PENTEKOSTE GOSPEL MISSION lililopo Kibaha kwa ulaghai wa kutaka kupata waumini kwa kusingizia mchawi amedondoka kwenye maombi ya mkesha wake na waumini.

Wamewashikilia kwa mahojiano kutokana na taarifa za mtu mmoja jinsia ya kiume Basenga Silvester Matheo (59) kudondoka kanisani akiwa anasafiri kwa ungo wa kichawi au kishirikina.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha mkoani Pwani, Kamanda wa Polisi ACP Pius Lutumo amesema, tarehe 24 mwezi huu majira ya saa 09:00hrs huko katika kituo cha polisi Kibaha Mkoa wa Pwani alitoa taarifa za mtu mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Basenga Silvester Matheo (59) mkazi wa Miswe wilaya ya Kibaha akiwa amesafiri kwa ungo wa kishirikina na
kudondoka kanisani hapo na kuleta taharuki kubwa kwa waumini.

Katika uchunguzi, jeshi la polisi lilibaini kuwa tukio hilo ni tukio la kutengeneza kwa lengo la kuwalaghai au kuwahadaa waumini na wananchi kwa ujumla kwa lengo la kupata waumini zaidi na kujipatia kipato.

“Ilielezwa kwamba siku ya tukio kulikuwa na ibada ya mkesha ambapo mtuhumiwa akiwa na wenzake sita alidondoshwa kwa sala za maombi ya waumini na mchungaji wao na wenzake wakafanikiwa kutoroka kichawi”.

“ili kudhibiti taharuki hiyo
mchungaji alimchukua mtu huyo na vifaa vyake vya kishirikina na kumuweka ofisini kwake hadi asubuhi polisi walipofika na kumchukua”

Bwana BUSENGAS/OSILVESTER MATHEO alijinisibu kuwa yeye na wenzake walifika kanisani hapo kishirikina kwa lengo la kupima imani ya waumini
hao kwa Mwenyezi Mungu.

Aidha mtuhumiwa aliahidiwa kulipwa Shilingi 50,000/= baada ya kutimiza lengo lao la kilaghai.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linatoa onyo na tahadhari kwa watu wenye tamaa ya
kupata kipato cha haraka kwa kufanya ulaghai kuacha mara moja.

Aidha linatoa wito kwa waumini kuwa makini na watu wachache wanaotaka kuharibu imani za
kidini kwa tamaa ya kipato

Previous articleTUTAJENGA SHULE KUMBUKUMBUKA YA PROF. DAVID MASAMBA MUSOMA VIJIJINI
Next article“TANZANIA IMEFANIKIWA KUTOKOMEZA MARBURG KUTOKANA NA UONGOZI MAHIRI WA RAIS SAMIA”- UMMY

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here