Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi David Silinde, amewataka wauzaji wa viuatilifu kuwa na takwimu pamoja majawabu yenye kujitoshekeza ili kuweza kuwasaidia wakulima wavuvi na wafugaji ili kuweza kuleta mageuzi katika sekta hizo
Rai hiyo ameitoa alipotembelea mabanda ya wakulima na wafugaji katika moenesho ya Nanenae Kanda ya Mashariki ambapo amesema takwimu hizo sahihi zitaweza kusaidia kuleta uzalishaji wenye tija.
Kwa upande wao baadhi ya wauzaji wa dawa na viuatilifu wanasema, jamii kushikilia matumizi ya viuatilifu kwa njia ya asili ni moja ya changamoto zinazowakabili katika utoaji elimu kwa wakulima na wafugaji