Home KITAIFA WATUHUMIWA MAUWAJI YA DK ISACK, MILEMBE WAKAMATWA

WATUHUMIWA MAUWAJI YA DK ISACK, MILEMBE WAKAMATWA

 

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema limefanikiwa kuwakamata watu watatu wanaotuhumiwa kumuua Dk Isack Daniel Athuman.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa jeshi hilo SACP David Misime imesema watuhumiwa hao watatu wamekamatwa mkoani Mwanza baada ya kufanya mauwaji ya Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya cha Karende kilichopo Tarime Rorya wakati akitoka kazini.

Jeshi hilo limeeleza baada ya watuhumiwa kutenda kosa hilo walikimbilia Mwanza na kisha mkoani Dar es Salaam ambapo askari wa uchunguzi waliwabaini na kuwakamata.

Taarifa hiyo imebainisha kuwakamata watuhumiwa watatu waliohusika kumuua mfanyakazi wa GGM Milembe Seleman Hungwa April 26,2023 na uchunguzi zaidi unaendelea ili kuwafikisha mahakamani.

Previous articleWAZIRI MKUU MAJALIWA AOMBA KUSITISHWA MGOMO KARIAKOO
Next articleWAZIRI GWAJIMA AWATAKA WAZAZI KUWALINDA WATOTO WAO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here