Home KITAIFA WATU WANNE WA FAMILIA MOJA WAFARIKI KWA KUVUTA MOSHI WA JENERETA DAR...

WATU WANNE WA FAMILIA MOJA WAFARIKI KWA KUVUTA MOSHI WA JENERETA DAR ES SALAAM

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza tukio la vifo vya watu wa nne wa
familia moja ambao wamepoteza maisha baada ya kuvuta hewa chafu ya moshi kutoka kwenye jenereta walilowasha ndani ya nyumba na baadae kulala.

 

Tukio hilo la kusikitisha limetokea siku ya tarehe 18. 04. 2023 majira ya saa 4:00 usiku baada ya watu hao kuwasha jenereta mara baada ya umeme kukatika kisha kuliweka ndani ya nyumba.

 

Uchunguzi wa awali wa Jeshi hilo unaoneshakuwa watu hao walipoteza maisha baada ya kuvuta hewa inayodaiwa kuwa ni hewa ya moshi iliyokuwa inatoka kwenye jenereta baada ya kuwashwa.

 

Watu waliopoteza maisha ni Kazija Mohamed (21), Munir Ibrahim(7), Munira Ibrahim(6), Muyyat Ibrahim (3). Huku Mume na mke Ibrahim Juma (28) na Aisha Ayubu(29) wote wakazi wa Kilimahewa, Chang’ombe wanapatiwa matibabu ambapo inaelezwa hali zao sio nzuri na wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali
Taifa ya Muhimbili.

Previous articleKAIMU MENEJA WA TANROADS TABORA: MRADI WA BARABARA YA KAZILAMBWA-CHAGU KWA KIWANGO CHA LAMI KUWEZESHA USAFIRI NA USAFIRISHAJI KATI YA TANZANIA NA NCHI JIRANI
Next articleWIKI YA UBUNIFU KUFANYIKA DODOMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here