Home KITAIFA WATU NANE WAFARIKI KWA AJALI YA GARI, KIBONDO KIGOMA

WATU NANE WAFARIKI KWA AJALI YA GARI, KIBONDO KIGOMA

Watu nane (8) wanadaiwa kufariki Dunia kufuatia ajali ya gari iliyotokea jioni ya leo, Jumamosi Desemba 23.2023 wilaya ya Kibondo, mkoa wa Kugoma

Ajali hiyo ambayo imehusisha magari mawili, Probox ya abiria inayofanya safari zake kati ya wilaya ya Kibondo na Kakonko na roli aina ya Sharkman inayomilikiwa na Kampuni ya Chiko (Kampuni ya Wachina wanaotengeneza Barabara) katika eneo la Kijiji cha Kumkugwa (Kilemba)

Mashuhuda wameieleza Jambo TV kuwa chanzo kilichopelekea ajali hiyo ni mwendokasi na uzembe wa Dereva wa gari dogo ambaye inaelezwa kuwa alitaka kuipita bila tahadhari gari inayomilikiwa na Kampuni ya Chiko ambayo kwa wakati huo iikuwa kambini kwao (sehemu waliyoweka Kambi kwa ajili ya Ujenzi wa Barabara), hali hiyo ikapelekea Probox kuingia ubavuni mwa roli na hatimaye gari zote mbili kupinduka,

Jambo TV itaendelea kukupatia taarifa zaidi kuhusiana na ajali hiyo

Previous articleACT WAZALENDO KUWAVUTIA MABINTI
Next articleMWENEZI CCM ILEJE AONYA WALAJI FEDHA ZA MIRADI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here