Jeshi la polisi Mkoani Tanga linawashikilia watu 11 waliokuwa wameweka kambi jijini Tanga na kuendesha wizi kwa njia ya simu katika mikoa mbalimbali nchini
Watuhumiwa hao ambao walikuwa wamepanga nyumba katika mtaa wa Donge jijini Tanga na kulipa kodi ya sh 800,000 wamekutwa na simu,line,jiko na chetezo kwa ajili ya kuchomea line na karatasi zenye namba walizolikwishatapeli na wanazotarajia kuendesha utapeli huo pamoja na fedha shilingi za Tanzania,Dola za Marekani na fedha za Congo DRC.
Fedha za kitanzania walizokutwa nazo ni sh 2,085,300,za Congo DRC sh 45,100 na dola moja ya kimarekani.
Akizungumza na Waandishi wa Habrai Mkoani hapa ,Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe amewataja waliokamatwa kuwa ni Hadija Nyange (34) mkazi wa Muheza,Zaina Athumani (25) mkazi wa Mwanzange,Innocent Omeme (35) wa Dar es salaam,Abdulaziz Nzori (31) wa Dar es salaam, Said Hassan (24) wa Dar es salaam, Rashid Habibu (23) wa Dar es salaam,Said Juma (30) ,Idd Kaniki (35),David Rupiana wa Dar es salaam (22),Omary Mohamed (27) wa Mkanyageni Tanga na Salum Rajab (24) wa Dar es salaam.
Hata hivyo watuhumiwa hao Walikutwa pia na kadi za simu,pikipiki,kadi za benki simu ndogo za tochi 13 maarufu kiswaswadu ,simu 11 kubwa za smartphone.
MWISHO