Home KITAIFA WATATU WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUJERUHI, KUPORA WATU DARAJA LA SALENDA

WATATU WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUJERUHI, KUPORA WATU DARAJA LA SALENDA

 

NA JESHI LA POLISI, DAR ES SALAAM

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu watatu kwa tuhuma za kujeruhi na kupora watu vitu mbalimbali katika maeneo ya daraja la salenda eneo la mikoko. Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Ya Dar es Salaam, SACP. Muliro J. Muliro amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia ufuatiliaji mkubwa wa wahalifu wanao jihusisha na matukio ya namna hiyo.

Aidha Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na ufuatiliaji wa wahalifu wanaopora kwa kutumia pikipiki katika maeneo mbalimbali ya Jiji, na Jeshi la Polisi litawakamata na baadae kuwafikisha katika vyombo vingine vya kisheria kwa hatua zaidi.

Previous articleWANAOTAKA KUMPINDUA RAIS SAMIA WAONYWA_ MAGAZETINI LEO JUMAMOSI AGOSTI 12 /2023
Next articleRAIS SAMIA AFANYA MAGEUZI MAKUBWA MIRADI YA MAENDELEO BUKOMBE-DKT BITEKO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here