Jumla ya Watanzania 200 wakiwa wanaondoka katika uwanja wa ndege Sudan na kurejea nchini kufuatia mapigano yanayoendelea nchini humo baina ya kikosi cha Jeshi la Sudan (SAF) na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).
Idadi hiyo inahusisha wanafunzi 150, watumishi wa Ubalozi 28, diaspora 22.
Wamo pia raia wa nchi za Marekani, Uingereza, Kenya, Uganda, Sierra Leone, Malawi, Zambia na Msumbiji ambao.
Wote kwa pamoja walisafirishwa kwa mabasi kwa siku mbili kutoka Khartoum, Al Qadarif, Metema hadi Gondar zaidi ya kilometa 900.
Baadae walisafirishwa kwa ndege ndogo toka Gondar hadi Bole walikochukuliwa na ndege ya ATCL hadi Dar es Salaam, Tanzania.