Home KITAIFA WATANO WANUSURIKA KIFO MOROGORO

WATANO WANUSURIKA KIFO MOROGORO

Watu watano wamenusurika kifo baada ya basi aina ya yutong yenye namba za usajili T 279 DZX kampuni ya Ester iliyokuwa ikitokea Dar-es-salaam kuelekea Singida kugongana na bajaji ambayo haikuwa na namba za usajili maeneo ya kihonda mbuyuni barabara kuu ya kuelekea Dar-es-salaam.

Kaimu mganga mfawidhi hospitali ya rufaa Mkoa wa Morogoro Abilahi Issa amekiri kupokea majeruhi hao ambapo anasema,majeruhi waliopokelewa ni watano kati yao wanne jinsia ya kiume na mmoja jinsia ya kike na wengi wamevunjika mifupa miguuni na sehemu za kichwa.

Kaimu kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro Hassan Omary amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema ,chanzo cha ajali ni dereva wa basi kujaribu kuyapita magari mengine na kusababisha ajali hiyo hivyo jeshi la polisi linamshikilia dereva huyo.

Previous articleRAIS SAMIA MGENI RASMI MAADHIMISHO JKT.
Next articleBAADA YA MIAKA 12 DAVID DE GEA AMETHIBITISHA KUONDOKA MANCHESTER UNITED

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here