Home KITAIFA “WATAALAMU WA HALMASHAURI PELEKENI KISARAWE MLICHOJIFUNZA NANENANE”_ DIBIBI

“WATAALAMU WA HALMASHAURI PELEKENI KISARAWE MLICHOJIFUNZA NANENANE”_ DIBIBI

 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya Kisarawe Ndugu Hamis Dibibi amewataka Wataalamu wa halmashauri wilaya Kisarawe kwenda vijiji kwa ajili ya kutoa msaada kwa wakulima na wadau mbalimbali walichojifunza kwenye Maadhimisho ya Nanenane mkoani Morogoro.

Amesema hayo Akizungumza kwa niaba ya Wajumbe wenzake wakati wa kilele cha Maonesho ya wakulima, Wavuvi na Wafugaji Kanda ya Mashariki ambapo Wajumbe wa Sekretariet kuu na Madiwani wa Baraza la Madiwani wa Wilaya ya Kisarawe walipo tembelea banda la Halmashauri hiyo lililopo morogoro katika Viwanja vya Julias Kambarage Nyerere.

Dibibi alisema waliofika hapo amefurahishwa na mandalizi ya kuonyesha shughuli mbalimbali za kilimo, Mifugo na Uvuvi hivyo amewataka wataaalamu wa halmashari wilaya Kisarawe kwenda vijiji kwa ajili ya kutoa msaada kwa wakulima na wadau mbalimbali ili Wananchi wapate tija katika uzalishaji wao wa kila siku.

“*hivi vipando vya hapa morogoro hata kule kisarawe inawezekana sana tu wito wangu zaidi wataalamu watumie nafasi zao kufanya kazi mashambani waliko wakulima na wadau mbalimbali wa kilimo na ufugaji kwa vitendo” amesema Dibibi.

“Wito wangu ni kwa wataalmu wa halmashauri kwenda zile kata ambazo Kisarawe wametenga kwaajili ya kilimo, ufugaji kama vile kule Kata za Mafizi, Mzenga na Vikumburu kuliko kukaa Kisarawe mjini huku wao Wananchi wakisuriri huduma zao vijijini” amesema Dibibi

“Wilaya ya Kisarawe asilimia kubwa ardhi yake ina rutuba ya kutosha basi Wataaalamu tumieni fursa hiyo kutoa msaada kwa Wakulima hata Wakulima walime mazao ya kimkakati kama ufuta, mahindi, muhogo na nazi ili kuwa na kilimo cha biashara pia wajipatie kipato badala ya kilimo cha chakula pekee amefafanua Dibibi.

Maonesho ya mwaka huu kitaifa 2023 yamefanyika mkoani Mbeya na Mgeni rasmi ni Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo katika Maonesho ya Kanda ya Mashariki yakifungwa na Rais mstaafu Mhe Jakaya Kikwete na kauli mbiu ya mwaka huu ni vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula.

 

Previous articleKMC YAMPA MKONO WA KWA HERI CHRISTINA MWAGALA
Next articleWANAFUNZI 322 WAHITIMU LUHETI MKOANI NJOMBE,MBUNGE KAMONGA AWATAKA WAKAHESHIMU VIAPO VYAO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here