Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. David Silinde ,amesema serikali imeanza kufikilia kuwaalika wakulima na wataalamu wa kilimo na mifugo kutoka katika nchi jirani na Tanzania ili kushiriki katika maonesho ya kilimo, mifugo na uvuvi yanayoendelea katika viwanja mbalimbali ili watanzania waweze kujifunza mbinu zinazotumiwa na mataifa hayo
Silinde amesema hayo wakati alipotembelea maonesho ya 30 ya nanenane kanda ya mashariki katika viwanja vya mwalimu Julius Nyerere Mkoa wa Morogoro ambapo amesema ili kuongeza tija kwa wakulima katika maonesho hayo ni wakati sasa wa kuwaalika mataifa kama Zambia, Msumbiji, Randwa na Burundi ili kujua taaluma wanayotumia katika kilimo chao
Aidha Silinde amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo ili waweze kujifunza pamoja na kuwekeza kisasa katika sekta muhimu za kilimo,uvuvi na ufugaji.