Home KITAIFA WATAALAM NCHI JIRANI KUALIKWA KATIKA MAONESHO YA 88 YANAYOENDELEA NCHINI

WATAALAM NCHI JIRANI KUALIKWA KATIKA MAONESHO YA 88 YANAYOENDELEA NCHINI

 

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde amesema, serikali imeanza kufikiria kuwaalika wakulima na wataalamu wa kilimo na mifugo kutoka katika nchi jirani na Tanzania ili kushiriki katika maonesho ya kilimo, mifugo na uvuvi yanayoendelea katika viwanja mbalimbali ili watanzania waweze kujifunza mbinu zinazotumiwa na mataifa hayo

Silinde amesema hayo wakati alipotembelea maonesho ya 30 ya Nanenane Kanda ya Mashariki katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Mkoa wa Morogoro ambapo amesema ili kuongeza tija kwa wakulima katika maonesho hayo ni wakati sasa wa kuwaalika mataifa kama Zambia, Msumbiji, Rwanda na Burundi ili kujua taaluma wanayotumia katika kilimo chao.

Aidha Silinde amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo ili waweze kujifunza pamoja na kuwekeza kisasa katika sekta muhimu za kilimo,uvuvi na ufugaji.

Previous articleMSONGO WA MAWAZO WATAJWA KUWA SABABU YA KUATHIRI AFYA YA WAJAWAZITO NA LISHE KWA WATOTO
Next articleMAKALI YA MAISHA KUPAA BEI ZA MAFUTA ZAPANDA, WASAFIRISHAJI WAITANA WAPANDISHE NAULI_ MAGAZETINI LEO ALHAMISI AGOSTI 03/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here