VIONGOZI wa dini na wasimaminzi wa ndoa nchini wametakiwa kutoa elimu ya malezi ya Mtoto kwa wanandoa kipindi cha uchumba ili kupunguza ukatili unatokea kwa asilimia 60 ndani ya familia.
Hayo yamsemwa julai 13, 2023 jijini Dodoma na Naibu katibu Mkuu wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Wakili Amon Mpanju wakati wa Mkutano wa Taifa wa wadau wa malezi na kutokomeza ukatili dhidi ya watoto.
Amesema ‘’Haiwezekani tunaviongozi wa dini wanafungisha ndoa, sasa kama tumewapa leseni ya kufungisha ndoa basi kwenye uchumba wawaandae vizuri wajue siyo kwenye ndoa wanaenda kustarehe tendo la ngono , wawaandae ili wajue majukumuu yao, hili ni jukumu la viongozi wa dini na wakimila, siyo wanafungisha ndoa wanaitupia serikali mzigo , je misingi ya kuwapata hawa wasiaminzi wa ndoa inafuatwa , siku hizi unamtafuta mtu kisa ni mweupe mnaenda basi anakuwa msimaminzi wakati huo yeye mwenyewe ndoa yake inamshinda atakujaje kusimamia yakwangu,’’ amesema wakili Mpanju.
Amesema migogoro ndani ya familia inaathiri kizazi cha sasa na kijacho hii ni kutokana na changamoto kubwa ya ukosefu wa elimu ya malezi kwenye jamii, ambapo hupelekea kuongezeka kwa matukio ya ukatili ikiwemo watoto wa mitaani , ujambazi.
‘’Vitendo vya ukatili vilivyofanyika dhidi ya watoto kwa mwaka 2022 ni 12163, kati ya hivyo vitendo vilivyoongoza ni ubakaji 6335, vinafuatiwa na ulawiti ni 1557, watoto kupewa mimba katika umri mdogo 1555 saivi kuna kiwango cha ukatili kuongezeka kwa watoto wote wakiume na wakike ,’’ameongeza wakili mpanju.
Pamoja na hayo wakili Mpanju amewataka wadau wanaotekeleza afua za malezi dhidi ya Mtoto kushirikiana na Tamisemi hasa katika ngazi ya halmashauri ili kuandaa mkakati wa Ulinzi na malezi kwa mtoto na kuona namna zitakavyotatuliwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi kutoka Wizara hiyo Sebastian Kitiku amesema changamoto za malezi zipo nyingi na moja ya sababu zinazopelekea ni mwingiliano wa mila na desturi za jamii mbali mbali, na maendeleo ya teknolojia ya Habari.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo amewataka wazazi kupata nafasi ya kuzungumza na mtoto ili kujua kila changamoto anayopitia.