Home KITAIFA WANNE WAFARIKI KWA AJALI YA GARI BAGAMOYO

WANNE WAFARIKI KWA AJALI YA GARI BAGAMOYO

Magari mawili yamegongana na kusababisha watu wanne wamefariki dunia akiwemo Mkurugenzi wa benk ya APSA Nechi Msuya aliyekuwa akiendesha Prado huko kijiji cha Mapatano katika Kata ya Mbwewe mkoani Pwani saa 8:30 Usiku.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake Kibaha mkoani Pwani Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP Pius Lutumo amesema gari lenye namba za usajili T 104 CBU aina ya Toyota Prado likitokea Dar es Salaam kuelekea Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro likiendeshwa na Nechi Msuya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 45-50 ambaye ndio Mkurugenzi wa benki ya ABSA na mkazi wa jijini Dar es Salaam liligongana na scania lenye namba za usajili T 881 DWU/ T 888 DWU likitokea Arusha kuelekea Dar es Salaam.

Amesema Scania hilo lilikuwa likiendeshwa na Philipo Mtisi (43) mkazi wa Mafinga na kusababisha vifo vya watu wanne na uharibifu wa magari hayo.

Kamanda Lutumo amewataja waliofariki wengine kuwa ni Dayana Mageta mwenye umri wa miaka kati ya 40 – 45 mfanyabiashara na Mkazi wa Dar es salaam, Norah Msuya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka Kati 40 – 45 Mwalimu wa Chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Dar es Salaam.

“Mwingine ni abiria wa kike ambaye jina lake halikufahamika anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 -35”

“Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari namba T 104 CBU aina ya Toyota Prado kwa kuhama kutoka upande wa kushoto wa barabara kwenda upande wa kulia kisha kugongana uso kwa uso na Lori hilo aina ya Scania”

“Miili ya marehemu imehifadhiwa katika zahanati ya Lugoba kwa uchunguzi wa daktari na kukabidhiwa ndigu wa marehemu kwaajili ya mazishi”

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linatoa wito kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara kuchukua taadhari na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepukana na ajali zinazoweza kusababishwa na uzembe.

“Pia tunawataadharisha madereva kuacha kutumia vileo wanapoendesha vyombo vya moto kwani imekuwa ni chanzo cha kusababisha ajali za barabarani”

Previous articleMSIGWA ATOA TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA TIBA ASILI
Next articleTAASISI ZA KIFEDHA ZAOMBWA KUPUNGUZA RIBA KWA WAKULIMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here