Home KITAIFA WANAWAKE NJOMBE WAHIMIZWA KUTUMIA BIDHAA ZAO ILI KUKUZA UCHUMI WAO

WANAWAKE NJOMBE WAHIMIZWA KUTUMIA BIDHAA ZAO ILI KUKUZA UCHUMI WAO

 

Njombe

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Njombe ametoa rai kwa kwa wanawake mkoani humo kupenda zaidi kutumia bidhaa zao za ndani kuliko za nje ikiwemo sabuni zao (Mama soap) zinazotengenezwa Jumuiya yao ili kuunga mkono,kukuza na kuinua uchumi wao kwanza.

Amebainisha hayo mara baada ya kuzindua kikundi cha Binti CCM wilaya ya Ludewa chenye wasichana zaidi ya 30 ambao ni zao la UWT wenye malengo mbali mbali ikiwemo ya kusaidia makundi mbali mbali kwenye jamii,kuhamasisha na kukisemea vizuri Chama,na kufanya biashara ndogo ndogo kupunguza utegemezi.

“Kwa kuwa mmesema malengo yenu pia kufanya biashara ndogo ndogo niwaombeni sasa mkauze na hizi sabuni Mama soap Number one,mvipendeni hivi vya kwenu kwanza kwa kuwa hii sabuni inatengenezwa na UWT mkoa wa Njombe ambao ndio nyie kwa kuwa ni maono ambayo tuliyasema sasa tunatekeleza na uchumi wetu utakuwa kwa sababu siasa inaenda na uchumi”amesema Scolastika Kevela

Awali katibu wa UWT wilaya ya Ludewa Magreth Chiwango ameeleza malengo ya kundi hilo kwa Jumuiya na Chama.

“Lengo letu la kwanza ni kuendelea kuhakikisha Chama chetu kina shika dola,kuhakikisha mama Samia anasemewa vizuri mitaani,kusaidia jamii lakini pia tumepanga kuwa na biashara zetu ili tusiwe tegemezi”amesema Chiwango
Kwa upande katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa Gervas Ndaki amesema ujumbe walioupata kupitia tukio hilo unakwenda kufanyiwa kazi ili uweze kuwafikia wanachama wa kutosha.

“Jumbe ambazo tumezipata hapa tutaendelea nazo mpaka kwenye ngazi ya kata,tunataka tunapofika kwenye uchaguzi tuwe na nguvu ya kutosha”alisema Ndaki

Kwa niaba ya Mabinti CCM katibu wa UWT wilaya ya Ludewa Magreth Chiwango wamemshukuru mwenyekiti wa UWT kwa kufika na kuzindua kundi hilo ambapo wameahidi pia kutumia na kuuza bidhaa ya sabuni yao huku pia wajumbe wengine wa UWT waliojifunza utengenezaji wa sabuni wakishukuru kupata mafunzo na kuahidi kushirikiana ili kukuza bidhaa hizo.

Previous articleMAAFISA ELIMU WAAGIZWA KUSIMAMIA UJENZI WA MIRADI YA ELIMU USIKU NA MCHANA.
Next articleBINTI ALIYETOWEKA SIKU 36 APATIKANA KWA MUUZA MKAA_ MAGAZETINI LEO JUMAMOSI JUNI 24/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here