Home KITAIFA WANAWAKE 400 WAPEWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

WANAWAKE 400 WAPEWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

 

Na Husna Hassan,Mtwara.

Mjumbe wa Halmashauri kuu Mkoa wa Mtwara Mohamed Abdallah ambae ni mgeni rasmi kwenye Mafunzo ya wajasiriamali wanawake,amewaomba wanawake wa kata ya Vigaeni iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara kuyatilia mkazo mafunzo waliyoyapata ili kuhakikisha wanazidi kukuwa kiuchumi.

Mohammed ameyasema hayo leo August 31,2023 wakat wa kufunga mafunzo ya wajasiriamali wanawake yaliyo wakutanisha wanawake 400 yenye lengo la kutoa elimu ya biashara ili kumkomboa mwanamke kiuchumi.

Sambamba na mafunzo hayo Mohammed ametoa Msada wa vifaa na pesa vilivyo gharimu zaidi ya shilingi milioni 6 kwa vikundi vya wanawake wajasiriamali ambavyo ni kikundi cha wanawake wajane(Tegemeo),Mipango,Nguvu kazi na kikundi cha mboga mboga ili kuendeleza na kukuza miradi yao.

Aidha amewaomba wanawake hao wanapofanikiwa katika maisha wasiwadharau waume zao.”niwaombe kina mama mujue umuhimu wa familia uchumi wenu unapokuwa basi tusidharau na ndoa zetu nyumbani bila baba nyumbani hakuna ndoa bila ndoa hakuna stara.”amesema Mohammed

Nae Diwani wa Kata ya Vigaeni Said Ally Nasoro ambae ndio muaandaaji wa mafunzo hayo amesema kuwa lengo kuu la kuandaa mafunzo hayo kwenye kata yake ni kutokana na wanawake wengi kutokuwa na elimu ya Ujasiriamali hali ilomfanya kuwakutanisha wanawake hao ili kuwaongezea elimu na ujuzi zaidi kuhusu biashara.

Kwa upande wake Muwezeshaji wa mafunzo hayo Joel Nanauka amesema elimu hiyo imemlenga mwanamke zaidi kwenye kuanzisha,kukuza,kupanua biashara na kuwaimarisha wanapokutana na changamoto yoyote kwenye biashara kujua namna ya kutatua na ameongeza kuwa changamoto kubwa inayowakumba wajasiriamali ni kuingia kwenye biashara bila ya kuwa na maarifa.

 

Previous articleKIKWETE AWATAKA WADAU KUTIMIZA AHADI ZAO ZA KUISAIDIA SERIKALI KATIKA SEKTA YA ELIMU.
Next articleHURUMA YA DKT. SAMIA YAWAGUSA 13,000, NI WALE WA VYETI FEKI , PSSSF YA WALIPA BIL.35/- MAGAZETINI LEO IJUMAA SEPTEMBA 01/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here