Home KITAIFA WANAOFANYA NGONO YA MDOMO HATARINI KUPATA KANSA YA KOO

WANAOFANYA NGONO YA MDOMO HATARINI KUPATA KANSA YA KOO

 

Daktari bingwa wa Mfumo wa Masikio Pua na Koo (ENT) wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kati Benjamin Mkapa, Dkt. Faustine Bukanu amesema kufanya ngono kwa njia ya mdomo humweka mhusika katika hatari ya kupata maambukizi ya Virusi vya Papiloma.

Dkt. Bukanu amesema kuwa, kunyonyana ndimi (kupigana denda), kunyonyana viungo vya uzazi na migusano mingine ya aina hiyo ni njia inayoweza kumpa mtu maambukizi ya virusi vya Papiloma katika Koo na kuathiri mfumo wa Sauti huku akikabiliwa na uwezekano wa kupata ugonjwa wa Kansa ya Koo.

“Virusi hivyo hutengeneza vivimbe mithili ya vipele kwenye Koo na kusababisha mgonjwa kukosa Sauti, na wengine wanaweza kukumbwa na maradhi ya Saratani ya Koo” Alisema Dkt. Bukanu.

Kama ilivyo kwa Virusi vingine, taarifa za kitabibu zinaonesha kuwa hakuna tiba ya Kirusi cha Papiloma isipokuwa kuna kinga inayotolewa kwa vijana wanoingia katika umri wa utu uzima (vijana balehe).

“Kimsingi hakuna namna ya kumwondoa Kirusi huyo, isipokuwa tunatibu athari zake, Mfano, kwa mtu aliyekosa Sauti tutafanya Upasuaji wa njia ya Koo ili kuondosha vivimbe, kwa aliyepata Kansa ya Koo yeye hupatiwa matibabu ya dawa za Saratani au Miyonzi”

Dkt. Bukanu anafafanua kuwa, Virusi vya Papiloma huweza kuambukizwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Mtoto aliyezaliwa na maambukizi ya Papiloma hukabiliana na changamoto ya Kushindwa Kupumua vizuri, kupoteza sauti na kukohoa kikohozi kikavu mara kwa mara.

Jamii inapewa wito wa kujilinda dhidi ya ngono zembe, na wanapoona kuna vivimbe kama vipele kwenye viungo vyao vya uzazi waonane na madaktari mapema.

Previous articleBENKI YA DUNIA YAIPONGEZA TANZANIA KWA KUTEKELEZA MASUALA YA JINSIA
Next articleDUWASA KUTUMIA ZAIDI YA BIL. 30 KUTEKELEZA MIRADI MINNE YA UCHIMBAJI VISIMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here