Wananchi wa Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara wamepongezwa kwa kuanzisha benki ya kijamii ya Tandahimba (Community Bank TACOBA)
Pongezi hizo zimetolewa Juni 24,2023 na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara Musa Saidi Nyengedi wakati akiongea na wanahisa wa benki hiyo kwenye mkutano mkuu wa 9.
Aidha Nyengedi amewaomba wananchi wa Tandahimba kuiunga mkono Benki hiyo ili kuishawishi Halmashauri na Wilaya jirani kutumia benk hiyo na kuleta utofauti na benki nyingine za Tanzania.
“Niwapongeze wananchi wa Tandahimba kwa kutoa dira na mwongozo mkubwa kwa Mkoa wa Mtwara kwa kuthubutu kuanzisha benk yenu ya ushirika.Pia kauli mbiu ya twende pamoja ni muhimu kweli niwaombe wakulima na wananchi tuitumie benki yetu,tuiunge mkono kwasababu huu ndo ukombozi wetu.”amesema Nyengedi
Nae Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanali Patrik Sawala akiongea kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanal Ahmed Abbas, amewaomba wana Tandahimba wote kuiunga mkono benki hiyo ya TACOBA hasa katika kipindi hiki ambacho inaendelea kujiimalisha kimkakati katika kuongeza ufanisi wake.
“Niwapongeze kwa namna mnavyoshirikiana kuhakikisha benki hii inakwenda kulingana na mchokipanga na mlicho kiazimia wanahisa,niwapongeze viongozi wa bodi kwa namna mnavyofanya kazi ili kuhakikisha malengo yenu yanafikiwa jitihada zenu zinaonekana.”
“Niwaombe wanahabari kufikisha ujumbe kwa watanzania wote juu ya uwepo wa benk hii ya wananchi Tandahimba TACOBA taarifa sahihibziende kulingana na maazimio.”amesema kanali Sawala
Benki ya TACOBA hufanya mkutano mkuu wa mwaka wenye lengo lakupitia taarifa mbali mbali za benki hiyo, ambapo huu ni mkutano mkuu wa tisa.