NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
Wananchi na vijana nchini wametakiwa kukemea kauli za kejeli, kuudhi na maneno ya dharau zinazotolewa na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) dhidi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Rai hiyo imetolewa na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Victor Makundi ambapo amesema kuwa, katika mkutano wa hadhara wa CHADEMA katika Mkoa wa Kagera wilaya ya Bukoba Makamu Mwenyekiti wa chama hiko, Tundu Lissu alitoa kauli za kejeli dhidi ya kiongozi wa Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Watanzania tunatambua Rais wetu ni Dkt. Samia hivyo hatupaswi kuona akitumana na watu wachache alafu sisi tunyamaze huku sio sawa tunapaswa kuungana kwa pamoja kupinga matendo haya yasiendelee” alisema Makundi.
Amesema kuwa, wananchi hawapaswi kukubali wala kuvumilia watu hawa kila siku wakawa wanadhoofisha juhudi kubwa anazozifanya Rais katika kuwaletea wananchi maendeleo.