Home KITAIFA WANANCHI WATAKIWA KUACHA KUFANYA SHUGHULI ZA KIBINADAMU KARIBU NA VYANZO VYA MAJI

WANANCHI WATAKIWA KUACHA KUFANYA SHUGHULI ZA KIBINADAMU KARIBU NA VYANZO VYA MAJI

 

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Bw. Abdallah Shaib Kaim, amewaasa wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu karibu na maeneo ya vyanzo vya maji ili kunusuru upotevu wa maji.

Wakati wa zoezi la upandaji miti katika bwawa la Mindu mkoani Morogoro kiongozi huyo wa mbio za mwenge amesema serikali inaendelea na mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuhifadhi mazingira na kutunza vyanzo vya maji.

Pia kiongozi huyo wa mbio za mwenge ameipongeza Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu kwa kutii agizo la serikali lililotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip  Mpango,likielekeza Bodi zote za maji kupanda miti zaidi ya milioni mbili.

Bwawa la Mindu ni miongoni mwa vyanzo vya maji 231 vinavyosimamiwa na Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu mkoani Morogoro, bwawa hilo linategemewa kwa asilimia 75 ya  wakazi wa Manispaa ya Morogoro.

Previous articleRAIS SAMIA ATOA MWEZI MMOJA KUSAINIWA VIBALI VYA MINARA
Next articleMAJAMBAZI WAVAMIA STUDIO YA RADIO WAKATI WA MATANGAZO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here