Home KITAIFA WANANCHI NYANGUGE MAGU WALALAMIKIA VITENDO VYA UNYANYASAJI VINAVYOFANYWA NA MWEKEZAJI

WANANCHI NYANGUGE MAGU WALALAMIKIA VITENDO VYA UNYANYASAJI VINAVYOFANYWA NA MWEKEZAJI

Mwananchi wa kitongoji cha Nyambilo kilichopo Kata ya Nyanguge wilayani Magu mkoani Mwanza wamemuomba Mkuu wa Wilaya hiyo Recho Kasanda kuwaonya walinzi wa mwekezaji wa kampuni ya Tangreen Agriculture limited kuacha kuwakamata watu na kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji ikiwemo kuwapiga kwa vigezo vya kuingia kwenye mpaka wa mwekezaji huyo.

Malalamiko hayo yametolewa na wananchi hao kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mkuu wa Wilaya hiyo kwa wananchi na kusikiliza kero hiyo inayowakabili ili iweze kutatuliwa.

Kufuatia malalamiko hayo Mkuu wa Wilaya hiyo Recho Kasanda akaingilia kati sakata hilo na kumesema, ili kutatua migogoro ya mpaka iliyopo kati ya mwekezaji wa Kampuni ya Tangreen Agriculture limited inayojishughulisha na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba na wananchi wa Kijiji hicho amesema, anatarajia kufanya ziara rasmi ya kuweka mipaka mipya ili kuondoa migogoro iliyopo hivi sasa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa Kijiji hicho , Miaga Joseph na Melesiana Makoye wamesema, kuwa walinzi wa mwekezaji huyo wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya unyanyasaji kwa kuwakamata baadhi ya wananchi pindi wanapofanya shughuli zao katika maeneo yaliyopakana na eneo hilo kwa kuwafungia ndani nakisha kuwapiga.

“Tunasikitishwa na vitendo vinavyofanywa na walinzi wa mwekezaji huyu kwani alivyokuja kuomba eneo hili tuliongea na kukubaliana tutaishi kwa upendo na amani bila kuwa na migogoro yoyote ila tunasikitishwa na vitendo tunavyofanyiwa na wafanyakazi wake,wamesema.

Naye Mwekezaji wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina moja la Mr Chen amesema, lengo la kuweka kampuni hiyo kwenye eneo hilo ni kutaka kuzalisha ajira kwa wananchi na Taifa liweze kunufaika na wala siyo kuleta migogoro kwa jamii kama ilivyotokea kwasasa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo, Hilali Elisha amesema, mgogoro huo umedumu kwa takribani miezi minne hivyo ni yvema utatuliwe ili kuondokana na sintofahamu kati ya wananchi wanaofanya shughuli zao za uvuvi ziwani kwa ajiri ya kipato ili kuendesha familia zao.

Previous articleJK AKUTANA NA KAMISHNA WA UMOJA WA ULAYA (EU)
Next articleVUTA NIKUVUTE SPIKA, MDEE AZIMIO UENDESHAJI BANDARI _ MAGAZETINI LEO JUMAPILI JUNI 11/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here