NA DENIS SINKONDE, SONGWE
Mkuu wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe Mhe. Farida Mgomi amewasihi wananchi kujitokeza Kwa wingi kwenye zoezi la uchangiaji Damu salama kwa hiari kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wanaopungukiwa damu.
Akizungumza na wananchi kwa njia ya redio ya jamii Ileje Fm akihamasisha uchangiaji huo mkuu Mhe. mgomi amesema tupo kwenye kampeni ya uchangiaji damu kwa mwaka 2023 kuanzia Juni mosi mpaka Juni 14 ,2023 hivyo tunatarajia kukusanya kiasi kingi Cha damu.
Mhe. Mgomi amesema tukiwa kwenye zoezi la uchangiaji damu tujiepushe na Imani potofu zinazoweza kusababisha zoezi kutofanyika Kwa matarajio yaliyokusudiwa.
“Matarajio yangu ni kwamba elimu mliyopewa na wataalamu kupitia redio Ileje Fm itakuwa chachu ya Kila mwananchi mwenye sifa kuweza kuchangia damu, sambamba na kuondokana na Mila ambazo zimekuwa kikwazo Kwa wananchi ambao wapo tayari kuchangia damu”, amesema Mhe.Mgomi.
Mhe.Mgomi amewataka wataalamu wa afya kuhakijisha wanatumia kampeni hii ,kulingana na umuhimu wake kwenye maisha ya binadamu wenye uhitaji wa damu salama.
“Kuna watu wanaogopa kuchangia damu wakidhani kufanya hivyo Kuna madhara yoyote kumbe si kweli ,msiogope tuungane Kwa pamoja tuokoe maisha ya wengine kupitia kuwasaidia damu salama”, amesema Mhe. Mgomi.
Mhe. Mgomi amesema.kwa kutambua uhitaji mkubwa wa damu kwa wilaya yetu ambapo tunahitaji kuchangia chupa 70 hivyo Kila mmoja ajitokeze kuhakikisha tunafikia lengo.
Kwa upande wake mganga Mkuu wa halmashauri ya Ileje Joyce Ongati amesema Kwa wilaya ya Ileje wanatarajia kukusanya chupa 70 Kwa siku 14 ambapo Kila siku chupa Tano zinatakiwa kukusanywa, niwaombe wananchi mjitokeze kwenye maeneo yaliyoainishwa.
“Jitokezeni kwenye vituo vilivyotengwa kwa ajili ya zoezi hili kwani huduma hii inatolewa bure,ili tuokoe maisha ya mama mjamzito ,mtu atakayekuwa na uhitaji wa damu”, amesema Ongati.
Ujumbe wa muhimu 👇
“CHANGIA DAMU UOKOE MAISHA YA MTU USIYEMJUA LEO KAMA AMBAVYO WEWE UTAKAVYOOKOLEWA KUTOKA KWA MTU USIYEMJUA”.