Home KITAIFA WANAHABARI KILIMANJARO WAFUNGA OFISI,WASHINIKIZA KUSOMEWA MAPATO NA MATUMIZI

WANAHABARI KILIMANJARO WAFUNGA OFISI,WASHINIKIZA KUSOMEWA MAPATO NA MATUMIZI

 

KLABU ya Waandishi wa Habari mkoa wa Kilimanjaro (MECKI) imefungwa kwa kile kinachotajwa viongozi wa klabu kukiuka katiba ya chama hicho kwa kushindwa kufanya mkutano mkuu kwa zaidi ya miaka mitatu sasa huku hoja ya taarifa ya fedha ikionekana kuwa mwiba kwa viongozi hao.

Wakati wa zoezi la kufunga ofisi hizo zilizoko jirani na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Moshi baadhi ya wanachama na wasio wanachama wamesikika wakieleza kuchoshwa na taarifa za kuhairishwa mara kwa mara kwa ombi lao la kufanyika kwa mkutano mkuu wa dharura kujadili masuala ya klabu hiyo.

Katika ofisi hizo majira ya saa 9:00 alasiri wanachama hao walifika ofisini hapo na kumkuta Mratibu wa klabu na kumueleza nia yao ya kufika ofisini hapo baada ya kutia saini kitabu cha wageni.

“ Tumekuja hapa baada ya kuona maazimio tuliyokubaliana kwenye mkutano uliopita hayajatekelezwa hadi sasa na siku 21 tulizotoa zimemalizika.” alisema Gift Mongi.

Alisema maeneo ambayo yamekuwa yakiohojiwa zaidi ni kwenye mapato na matumizi pamoja na matumizi ya vifaa vya ofisi.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoani Kilimanjaro Bahati Mustapha amesema kuwa hajapata taarifa hizo.

“Kwasasa sijapata hizo taarifa naomba niwasiliane na viongozi wengine wa Klabu ya wanahabari kufahamu zaidi” alisema Bahati.

Previous articleAJALI YAUA WATANO NA KUJERUHI 20 MIKUMI MOROGORO.
Next articleWADANGANYA , WATUMIA VYETI FEKI KUOMBA AJIRA _MAGAZETINI LEO JUMANNE JUNE 06/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here