Home KITAIFA WANAFUNZI ZAIDI YA 1000 WAPIGWA MSASA WA BOOM

WANAFUNZI ZAIDI YA 1000 WAPIGWA MSASA WA BOOM

 

Wanafunzi zaidi ya elfu moja ambao wanatarajia kujiunga na elimu ya juu ya vyuo vikuu wametakiwa kutumia vizuri fedha za mkopo wanaopaitwa na serikali ili kujiepusha kujiingiza katika vitendo visivyofaa vikiwemo makundi mabaya

Akiwa katika warsha ya mafunzo ya kuwaandaa na kuwapatia uzoefu wanafunzi wa kidato cha sita na wale wanatajaria kujiunga na elimu ya juu Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Rebecca Nsemwa amesema ,kumekuwa na matatizo mengi pale mwanachuo anapomaliza mkopo (boom).

Amesema ni wakati sasa wa kuwapatia elimu ya matumizi ya fedha kabla ya kujiunga na elimu ya juu kwani wanafunzi wengi hawana elimu hiyo na pale wanapopata fedha ya mkopo kwa mpigo wanashindwa kujipangilia hivyo wanajikuta wanafanya vitendo viovu.

Kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi ya piga kitabu unit John Minja amesema
,ukosefu wa elimu pamoja na mabadiliko ya kimaisha yanayowatokea wanafunzi wanapofika vyuoni ndio sababu iliyowasukuma kuanzisha warsha ya mafunzo kwa wanafunzi hao.

Previous articleRAIS SAMIA ATAKA MAGEUZI YA KIFEDHA KIMATAIFA _MAGAZETINI LEO JUMAMOSI AGOSTI 26/2023
Next articleKAMA UNASUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI, HILI NDIO SULUHISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here