NA DENIS SINKONDWE, SONGWE.
MKUU wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe Mhe.Farida Mgomi amewahimiza wanafunzi wa shule za msingi mkoani humo kushiriki mashindano ya michezo mbalimbali Kwa lengo la kujifunza uzalendo.
Mhe. Mgomi amesema hayo Mei 19,2023 akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Songwe Mhe Dr Francis Michael wakati akifunga mashindano ya UMITASHUMTA ngazi Ya mkoa kwenye viwanja vya shule ya sekondari Ileje.
Mhe. Mgomi amesema michezo inasaidia kuimarisha mwili, kujenga afya ya akili, uzalendo wa nchi hali ambayo inawasidia vijana kujiajili na kuwaingizia kipato.
“Nawasihi wanangu jihusisheni na michezo kwani mtajifunza kanuni bora sambamba na kuwajengea upendo baina ya wanamichezo”,amesema Mhe. Mgomi
Akimwakilisha Afisa elimu mkoa wa Songwe Michael Ligola ,afisa utamaduni wa mkoa huo Godfrey Msokwa amesema mashindano hayo ngazi ya mkoa yalijumuisha wanamichezo 537 huku michezo ya wanawake imekua Kwa Kasi.
Msokwa ametaja idadi ya wanamichezo Kila halmashauri kuwa Ileje 139, Mbozi 120, Momba 82, Songwe 95 na Tunduma 120.
Katika mashindano hayo wilaya ya Mbozi imeibuka mshindi wa jumla kati ya michezo yote iliyochezwa .