Home KITAIFA WANAFUNZI 633 KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA,KIBAHA MJI

WANAFUNZI 633 KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA,KIBAHA MJI

 

Na Byarugaba Innocent,Kibaha.

Jumla wa watahiniwa 633 leo Mei 2,2023 wanaanza safari ya kufanya kufanya mtihani wa kidato cha sita kama sehemu ya kujitathmini kwa Mafunzo waliyoyapata ndani ya miaka sita rasm tangu walipoanza kidato cha kwanza.

Huu ni mfululizo wa kujitathmini kwao kwani miaka miwili iyopita walifanya hivyo kitaifa wakiwa kidato cha nne na walifaulu kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita.

Katika idadi hiyo wapo watahiniwa rasmi 571 na watahiniwa wa kujitegemea 62 ambapo jumla ya mikondo 18 imeandaliwa kwa watahiniwa wote 633 amesema Edward Jidamva Afisa Elimu taaluma ,Kibaha Mji

Rosemary Msasi Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Mji Kibaha amesema watahiniwa wote wameandaliwa vema na walimu hivyo amemtaka kila mmoja mtahiniwa kuyatumia vema maarifa aliyoyapata kutoka kwa walimu.

Awali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amewatakia kila la kheri katika mtihani wao huku akiahidi kuwa Serikali yake itaendelea kuhakikisha inaandaa Mazingira bora katika safari yao kuelekea hatua za mbele ikiwemo vyuo vya ufundi,vyuo vya kati na vyuo vya Elimu y juu.

Mtihani huo utafikia tamati tarehe 22 Mei,2023 nchi nzima.

Previous articleDKT. SAMIA AWABANA WAAJIRI WABABAIFU.. MASTAA SIMBA WABADILI GIA _ MAGAZETINI LEO JUMANNE MEI 02/2023
Next articleSAKATA LA TWIGA CEMENT KUTAKA KUINUNUA TANGA CEMENT BADO KAA LA MOTO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here