Serikali imeendelea kuimarisha utoaji wa mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu pamoja na kushirikisha wadau kwa lengo la kuongeza wigo wa upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa za uhitaji.
Katika kufikia azma hiyo Serikali imetoa jumla ya Shilingi 652,176,079,647 kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ambapo Shilingi 652,176,491,647 kwa wanafunzi wanaosoma ndani ya Nchi,Shilingi 586,588,000 kwa Wanafunzi wanaosoma nje ya Nchi.”-Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda
Aidha kipitia mfuko wa SAMIA Scholarship,Shilingi 2,754,370,430 zimetolewa kwa wanafunzi 593 wenye ufaulu wa juu katika masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Hisabati au Afya na Sayansi Shirikishi katika ngazi ya Shahada”_ Prof.Adolf Mkenda.