Bodi ya Maji Bonde la Wami-Ruvu imeanza oparesheni ya kusafisha mito iliyopo mkoani Morogoro pamoja na kuwaondoa watu walioweka makazi ya kudumu katika maeneo ya madaraja na kusababisha uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji.
Katika oparesheni hiyo baadhi ya vijana wanaotumia madawa ya kulevya wamekutwa wakiwa wameweka makazi ya kidumu chini ya daraja la mto Morogoro ,ambapo vijana hao wameeleza sababu ya kuweka makazi katika eneo hilo ni kukosa sehemu za kuishi hali inayochangiwa na ugumu wa maisha.
Meneja wa rasilimali za maji Bodi ya Maji Bonde la Wami-Ruvu Martin Kasambala ,amesema zoezi hilo litakuwa ni endelevu katika maeneo yote ya vyanzo vya maji na vijana watakaokutwa katika maeneo ya vyanzo vya maji watapatiwa elimu pamoja na kutafutiwa shughuli mbadala.