Home KITAIFA WALIOVAMIA KIA KULIPWA FIDIA KUANZIA MWEZI HUU

WALIOVAMIA KIA KULIPWA FIDIA KUANZIA MWEZI HUU

Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Amiri Mkalipa amesema Rais wa Tanzania Dkt. Samia amekubali kuidhinisha Tsh. bilioni 11 kwa ajili ya kuwalipa fidia Watu ambao walivamia eneo la uwanja wa ndege KIA ambalo linamilikiwa na Serikali na kujenga nyumba za kuishi na mashamba ambapo wataanza kulipwa fedha hizo kuanzia mwezi huu.

DC Mkalipa amesema licha ya Wananchi hao kuvamia eneo hilo lakini Rais Samia ameona sio vizuri kuwaondoa bila kuwapa fidia itakayowasaidia kupata makazi mapya na kuendeleza maisha yao.

Mkalipa amesema hayo leo July 12,2023 wakati akiwasilisha utekelezaji wa Ilani Wilayani humo kwa mwaka wa fedha 2022 /2023, ambapo amemshukuru Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasani kwa fedha Za maendeleo alizowainishia ikiwemo fedha za mradi wa maji Tsh. bilioni 3.392.

“Rais Samia ameidhinisha pia fedha za ujenzi wa barabara ni bilioni 5.594, Elimu Sekondari ujenzi wa miundombinu ni bilioni 1.787, elimu msingi ujenzi wa miundombinu bilioni 1.669

“Tunampongeza pia Rais Samia kwa mbolea ya ruzuku”

Previous articleMKURUGENZI MTWARA DC ATETA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI
Next articleMIAKA 30 JELA KWA UNYANG’ANYI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here